Quantcast
Channel: Uganda Daily Eye
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20859

Watuhumiwa mauaji Pwani watajwa

$
0
0
MKAKATI wa kupata taarifa za wahalifu wanaosadikiwa kuhusika kwenye matukio ya mauaji mkoani Pwani umeanza kufanikiwa, baada ya wananchi wa mkoa huo, kuanza kuwaanika wale wote wanaotuhumiwa kuhusika na matukio hayo.

Mkuu wa Mkoa huo, Evarist Ndikilo wakati akizungumza na gazeti hili, alibainisha kuwa tayari Kamati ya Ulinzi la Usalama ya Mkoa huo wa Pwani, kupitia kikosikazi ilichounda kushughulikia matukio hayo, imeanza kuwafuatilia watu hao waliotajwa ili kuwachunguza na endapo watabainika watachukuliwa hatua.

Alisema tangu kuanza kwa matukio hayo, mkoa huo ulikuja na mikakati kadhaa ya kuyadhibiti ikiwemo kutoa namba za viongozi wa kamati hiyo ya ulinzi na usalama kwa wananchi, ili waweze kuwataja kiurahisi wahalifu waliohusika na matukio hayo.
"Kwa sasa kupitia kikosikazi tulichounda, tumeanza kuwafuatilia wale wote waliotajwa kuhusika kwenye maeneo yao, tukiwapata tutawachunguza na tukibaini kuhusika tutawachukulia hatua za kisheria," alifafanua.
Alisema mkoa huo, katika kipindi kifupi kumekuwa na matukio kadhaa ya uhalifu wa silaha na mauaji kupitia watu wanaotumia pikipiki wanaofanya uhalifu huo kuanzia mida ya saa moja jioni. Alisema matukio hayo yalitokea katika maeneo ya Kibiti na Ikwiriri na kusababisha vifo vya watu watatu.
"Ndio maana kamati yetu iliamua kuja na mkakati wa kupiga marufuku bodaboda zote kusitisha huduma kuanzia majira ya saa 12 jioni hadi saa 12 asubuhi ili kuzuia matukio haya," alifafanua.
Ndikilo alisema pia kwa sasa mkoa huo umeweka vizuzi katika maeneo kadhaa mkoani humo ikiwemo Kibiti, Bangu, Mbalanga, Ifakara Mjini na daraja la Mkapa ikiwa ni moja ya hatua za kuhakikisha usalama wa raia wa mkoa huo na mali zao.
"Nawaomba wananchi wanaotumia njia hii pamoja na wakazi wa Pwani watuvumilie kwa kipindi hiki cha hatua za mpito kwani tumelenga kuhakikisha kuwa tunawadhibiti wahalifu hawa na kuwahakikishia usalama wananchi," alisema.
Aidha, alitoa mwito kwa wananchi kuhakikisha wanatii vyombo ya dola pale wanapopewa amri ya kujisalimisha au kufunga biashara zao mapema, kwani vyombo hivyo hutoa amri hizo kutokana na taarifa muhimu za kitelijensia zinazohusu masuala ya usalama wa raia.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Onesmo Lyanga alisema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha linawadhibiti na kuwatia nguvuni wahalifu wote waliohusika na matukio hayo.
Aliwataka wananchi wa mkoa huo, kutoa taarifa mara moja pale wanapowatilia mashaka watu ili hatua za haraka zichukuliwe na kuokoa maisha ya watu na mali zao.
Hatua hizo za Mkoa wa Pwani zimechukuliwa kutokana na mtiririko wa matukio yanayoendelea ya mauaji ya wenyeviti wa vyama na serikali ngazi ya vijiji, huku wahusika wa mauaji hayo walionekana kutumia usafiri wa pikipiki.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20859

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>