WATU wawili Fuljence Mapunda, maarufu Mwanakotite (32), ambaye ni msanii wa muziki na Mnesa Sikabwe (39), mtayarishaji wa muziki,




Jana walidhaminiwa kwa Sh. milioni kila mmoja baada ya kufikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kusambaza wimbo wa kuudhi dhidi ya Rais John Magufuli kupitia mtandao wa U-Tube.
Washtakiwa walikana mashtaka hayo.
Washtakiwa wanaotuhumiwa walisambaza wimbo kupitia mtandao huo wenye maneno ya "Udikteta Uchwara' dhidi ya Rais Magufuli.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Dereck Mukabatunzi, alidai kuwa Agosti 15, mwaka huu, kwenye eneo la Manzese jijini, washtakiwa walisambaza wimbo huo kupitia mtandao wa U-Tube uliokuwa na maneno ya kuudhi dhidi ya Rais.
Hakimu aliwataka kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi inayotambuliwa; watakaosaini hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. milioni 10.
Washtakiwa walitimiza masharti hayo na kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 12.